Album: Yatupasa Kushukuru
Sayari sayari eh dunia
Mbona wanipa-a hofu nyingi ewe dunia
Yatokeayo kwako ewe dunia
Kila kukicha mambo hugeuka kuwa maovu
Inawezekana umezeeka dunia
Au wakaao ndani yako ndio wamezeeka
Kila ufikapo ni vilio, nifanyeje
Maafa yakadiri wengi dunia wazeeka
Sayari dunia, uliumbwa wapendeza
Lakini sasa, watupeleka wapi?
Tunahangaika, hatujui tuendako
Ni Mungu pekee, ajuaye
Njaa magonjwa yasiyotibika
Mambo yatisha ewe dunia waenda wapi
Kila mahali ni jawa twende wapi
Rotuba nayo imekwisha toweka sasa twende wapi
Hali ya maisha ni ngumu sana kwa wote
Matajiri na maskini, wote ni sawa
Uchumi wa dunia yote wayumba
Ona mataifa makubwa yote nayo, yatetereka
Sayari dunia, uliumbwa wapendeza
Lakini sasa watupeleka wapi
Tunahangaika hatujui tuendako
Ni mungu pekee, ajuaye
Sayari, dunia umechoka
Na wakaao ndani yako wote wamekuchoka
Hakuna mzazi awezaye kuvumilia
Kuona mwanawe anakatwa kichwa kwa ajili ya kafara
Damu za watu zimekua ni tamu
Nionavyo si kawaida ewe dunia.
Tuyaonayo yanatisha dunia
Na yajayo hatuyajui oh nahofu moyoni mwangu
Sayari dunia, uliumbwa wapendeza
Lakini sasa, watupeleka wapi
Tunahangaika hatujui tuendako ni mungu pekee ajuaye
rating 5.0 with 2 votes
2 favs
I love the songs especially sayari...the vocals? check.. - Mar 2015